|

Nissan ya Mdau ilivyofanywa Breki na Basi kutoka kusini Jana.


Jana majira ya mchana imeshuhudiwa ajali maeneo ya Temeke Sudani katika stendi ya zamani ya mabasi yaendayo kusini mwa Tanzania, Ajali hiyo ilihusisha Basi la Kampuni ya Mrisho Investment ambalo lili poteza Breki na hatimaye kwenda kulivaa gari dogo aina ya Nissan Safari, inayomilikiwa na Ndugu Shaaban N'gonde hadi kuitoa nje ya Barabara.

Katika Ajali hiyo hakukuwa na majeruhi yoyote zaidi ya gari hilo Gumu (Nissan) kupata michubuko na kubonyea kwa upande wa dereva.

 
 Hilo ndio basi la Mrisho Investment lililofeli brake na kugonga gari ndogo aina ya Nissan
 Gari aina ya Pajero likiwa limesukumwa hadi nje ya barabara baada ya basi hilo kufeli brake na kugonga gari ndogo hadi nje ya barabara
 Wadau wakiangalia ajali hiyo iliyotokea temeke jana
 Mwenye gari ndogo aina ya Nissan Safari, Shaaban Ng'onde (mwenye Tshirt Nyeusi) lililogongwa na Basi akielezea jinsi alivyoweza kusukumwa kutoka barabarani hadi nje ya Barabara na basi lililofeli brake na kupitiliza hadi kugonga gari lake.
Wakazi wa Temeke Wakiangalia basi lililoacha njia na kugonga gari ndogo aina ya Nissani hapo jana Temeke Sudani.Hakuna Aliyejeruhiwa wala Kuumia
Special Credit: Jovin Bachwa Blog.

Posted by Unknown on 9:23 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Nissan ya Mdau ilivyofanywa Breki na Basi kutoka kusini Jana."

Leave a reply

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...