Angalia Picha za Basi La Meridian Lililopata Ajali Leo Hii.
Bado Jamii ya Watanzania Imeendelea Kupoteza Wapendwa wao kutokana na Ajali za Barabani. Leo hii kumeshudiwa Ajali nyingine Mbaya ya Barabarani Ikilihusisha Basi la Kampuni ya Meridiani lilokuwa likitokea Rombo Kuelekea Dar Es Salaam, ambalo lilipata ajali na kupinduka Maeneo ya Mbwewe Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Watu kadhaa wamefariki dunia na majeruhi ni wengi, Pia Inasemekana dereva wa basi hilo alikuwa kanasa baada ya kubanwa huku ikiaminika ameshafariki.
Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali Pema.
