Kijana Mwenye Kipaji cha Ajabu, Atengeneza Taswira Mbali Mbali ndani ya Tikiti Maji.
Qian Wei Cheng, 21, Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Tsinghua, hivi karibuni alijikuta amekuwa maarufu sana kupitia internet baada ya kuzagaa kwa picha zake ambazo hutengeneza taswira ya maumbo ya vitu mbali mbali kwa kutumia Tikiti Maji.
Kawaida wapo wengi wenye vipaji vya kufanana na Cheng, ispokuwa anawazidi kwa kuifanya kazi ya kipekee kwani hatumiaa mashine ya aina yoyote katika utengenezaji huo zaidi ya Kisu na Kijiko.
