Kumbe Jacqueline Pentezel ni zaidi ya Mke Mwema.
Mume wa muigizaji Jacqueline Pentezel, Garder Dibibi amefunga na kumwagia sifa kem kem mkewe huku akielezea ya kwamba tangu achukue jiko hilo rasmi miezi 8 iliyopita hajawahi kuugusa msosi wa mama ntilie.
“Mke wangu ni zaidi ya mke, ni tofauti na watu wanavyomchukulia na ni mtaalamu wa jikoni. Sijutii hata chembe kumuoa,” alisema Gardner.
