Samaki Mkubwa kuliko wote avuliwa huko Norway.
Mvuvi Marco Liebenow alidhani ndoano yake imekamata Sub Marine ndogo kutokana na uzito wa Samaki huyo, ukubwa wake ulimfanya ashindwe kuingia katika boti ya futi 19.
Mvuvi huyo mwenye asili ya Kijerumani akiwa amepozi na samaki huyo aliyemkamata juzi baada ya purokushani ya muda mrefu. kwa sasa wanasubiri mamlaka husika zithibitishe kuhusu rekodi mpya ya samaki mkubwa zaidi kuvuliwa duniani.
