Shule ya "Makahaba" yashinda Kesi
Ile Shule ya Makahaba iliyofunguliwa nchini Hispania, imeshinda kesi iliyokuwa ikiikabili ambayo ilifunguliwa na wanaharakati mbali mbali wa maadili nchini humo. Katika utetezi wake imesema hata ukiangalia matangazo yake hayajawagusa watoto bali ni watu wazima, hayahamasishi ukahaba bali ujuzi wa mapenzi na pia kutatoka waalimu ambao wataweza hata kutumiwa na shule za kawaida katika kutoa elimu ya mahusiano na mapenzi.Pia wamesema imefika hatua Ukahaba ukatambulika kama ajira rasmi kwani unaajiri watu wengi kuanzi umri wa miaka 19 hadi 45. Mbali na hivyo waliowahi kuanza kozi ya DIPLOMA wamehakikishiwa nafasi nzuri zaid za ualimu pale watakapohitimu na kufaulu vizuri. Upande ulioshindwa kesi unajipanga kukata rufaa.
Posted by Unknown
on 5:19 AM. Filed under
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response