Kijana Ajipachika katika nyaya za umeme na kujiua.
Kijana mmoja Amejiua kwa kutumia umeme Alhamisi ya juzi baada ya kujitundika katika Line moja yenye umeme mkubwa huko Nakuru, Kenya.
Kwa mujibu wa mmoja wa mashahidi wa tukio hilo, Susan Wachukua, Mtu huyo alifika katika eneo hilo na kuanza kuvua nguo zake zote, isha akaanza kupanda juu ya nguzo hizo za umeme.
"Tulidhani ni kawaida yake kuvua nguo maana Emmanuel ana matatizo ya Akili" Alisema, Huyu kijana alikuwa mkimya sana na kabla ya mauti alikuwa anajishughulisha na shughuli za ufundi seremala.
Wafanyakazi kutoka shirika la Umeme nchini Kenya walifika mapema baada ya Mtu huyo kunasa lakini iliwabidi wakae muda mrefu kuwasubiri Polisi wafike ili wapate ruhusa ya kuushusha mwili huo kutoka juu aliponasa.
Wafanyakazi hao walilazimika kuzima umeme wa kanda nzima ili kuweza kuushusha mwili huo.
Posted by Unknown
on 9:11 PM. Filed under
Habari za Kimataifa,
Maisha,
Ujana
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response