Mke wa Usher Ashindwa Kesi ya Kuwatunza Watoto, Baada ya Kumpoteza Mtoto wao Mkubwa.
Wanandoa hao wa zamani walimaliza kesi ya muda mrefu iliyofunguliwa na Aliyekuwa Mke wa Msanii wa R&B Usher Raymond, Tameka Foster baada ya Kufariki kwa mtoto wao Mkubwa, Kile, 11 wakati akiwa anaogelea katika Pool, Tukio ambalo mwanamke huyo amesema ni uzembe uliochangiwa na Baba yao kutoweka watu maalum kwa ajili ya kuwaangalia watoto hao.
Mke huyo alikuwa anaiomba mahakama impe ruhusa ya kuwachukua watoto wawili waliobaki ambao kisheria walikuwa wanalelewa na Usher ili kuepusha madhara mengine na hasa ukizingatia Usher hana utaratibu wa kumweleza chochote kuhusu maendeleo ya watoto hao au wapi walipo na wanaangaliwa na nani.
Mama huyo alizodi kulalamika ya kwamba kuna kipindi, hasa alichofariki mtoto wao huyo, watoto hawakuwa katika uangalizi mzuri kwani walikuwa wameachwa na shangazi yake Usher ambaye hana Malezi mazuri.
Hata hivyo mahakama imeamuru uangalizi wa watoto hao ubaki kwa baba yao ingawa anatakiwa awe anahakikisha taarifa za mara kwa mara zinamfikia mama yao kuhusu wapi walipo na chini ya uangalizi wa nani.
Posted by Unknown
on 2:34 AM. Filed under
Habari za Kimataifa,
Maisha,
Muziki,
Wasanii
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response