|

Pedeshee wa ukweli Aibuka Dar , Anagawa Pesa Kama "PIPI" Kashazitoa kwa Abiria, Hospitali na Bado...!!!

Madereva wa Boda Boda na Bajaj wakigombania kujaziwa mafuta ya Bure, Gharama kwa Pedeshee.

Kupitia Radio moja Mjini hapa, wiki hii nzima amekuwa akizungumziwa Kijana wa Kitanzania ambaye ameonesha tabia ya aina yake kwa vitendo vya kugawa pesa na kutoa misaada ya fdha pasi na kutaka kufahamika wala kutangtazwa.

Jamaa huyo kashawahi kuwalipia nauli abiria woote ndani ya dala dala la Mbagala, pia amewahi kwenda hospitali ya mwananyamala na kuuliza kama wapo watu ambao wanadaiwa na wameshindwa kulipa kisha akawalipia wote na kuondoka zake.

Neema pia aliwaangukia madereva wa Boda Boda na Bajaj alipowatembelea katika kijiwe chao huku akiwa kaongozana na askari polisi wawili wenye silaha maana anatembea na mihela ya kumwaga na kisha akawajazia mafuta full tank madereva woote wa Kijiwe hicho.

Haya Usiombe akakukuta, ni mihela tu bila kuuliza.

Posted by Unknown on 11:52 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Pedeshee wa ukweli Aibuka Dar , Anagawa Pesa Kama "PIPI" Kashazitoa kwa Abiria, Hospitali na Bado...!!!"

Leave a reply

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...