Ugonjwa wa Kutoka na Magamba ya Samaki katika Ngozi wamtesa Kijana Huyu.
Pan Xianhang, 8, ni Mtoto mzaliwa wa nchini China ambaye Majirani zake wamempa jina la "FISH BOY" Kutokana na ngozi yake kuwa na Magamba mithili ya Samaki. Pan alizaliwa huko Wenling, China akiwa na aina ya Kipekee ya Ugonjwa wa ngozi ujulikanao kitaalamu kama Ichthyosis.
Kutokana na Tatizo lake Pan amelazimika kuwa anatumia Cream na mafuta ya aina mbali mbali ili kuifanya ngozi yake ibakie katika unyevu na kuzuia kukakamaa zidi kwani humpelekea kupata maumivu makali.
Msemaji kutoka katika Taasisi inayosaidia wagonjwa wa Ichthyosis, Liz Dale amesema hakuna tiba maalumu ya ugonjwa huo zaidi ya kuhakikisha ngozi inabaki katika hali ya unyevu muda wote kwa mafuta na lotion maalum.
Zaidi ya watoto 16,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na aina fulani ya Ichthyosis, Ingawa ya Pan ni zaida ya wengi wao. Madakari wanaendelea kuitafuta Tiba ya kuwatibu wagonjwa wa aina hiyo.
Posted by Unknown
on 10:27 PM. Filed under
Habari za Kimataifa
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0.
Feel free to leave a response