|

Binti Amwagia Mafuta ya Moto Mpenz wake baada ya Kumtelekeza na kuchukua mwanamke Mwingine.


Pengine hili linaweza likawa onyo na funzo kwa vijana ambao wamekuwa na mazoea ya  kuwa na mahusiano na wasichana kisha kutembea nao kwa kipindi kifupi na kuwaacha solemba.

Juzi mahakama ya Hakimu mkazi ya Karu huko Abuja, Nigeria imemhukumu kifungo cha Mwaka Mmoja Jela Bi Victoria Alonge baada ya kupatikana na hatia ya kumuunguza Mpenzi wake na Kumsababishia majeraha katika mwili wake kwa kutumia mafuta ya Moto.

Katika Utetezi wake, Victoria amesema hilo ni funzo kwa Mpenzi wake huyo aitwaye Roland baada ya Kuwa na Mahusiano naye kwa kipindi cha miaka Minne (4) halafu kumtoroka na kuja kuishi na mwanamke mwingine huko Abuja.

Victoria alikamatwa baada ya kutenda kosa hilo mnamo majira ya Saa 10 Alfajiri alipovamia nyumba ya Roland huku akiwa kalala na kumiminia mafuta hayo ya moto.

Posted by Unknown on 8:21 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Binti Amwagia Mafuta ya Moto Mpenz wake baada ya Kumtelekeza na kuchukua mwanamke Mwingine."

Leave a reply

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...