|

Tabia Hizi za Mazoea Humsababishia Mtu Matatizo ya Figo, Chukua Tahadhari.

Mchekeshaji De Don, akiwa hospitali baada ya kumchangia figo kaka yake.

Katika Pita pita ya kawaida ndani ya mitandao ya kijamii na Blogs, japo sina Elimu Kubwa ya Kidaktari nimeona si vibaya japo kuzitaja tu baadhi ya tabia ambazo sisi waswahili tumezijengea mazoea na kuona ni kawaida kumbe mwisho wa siku husababisha madhara katika Moja ya viungo vyetu muhimu, Figo.

Kwa uchache angalia tabia hizo ili nawe uziepuke au kuzipunguza, pia uwafahamishe uwapendao.:-

1. Kukaa na " Uchafu/Kinyesi" Muda Mrefu Tumboni
2. Kutokunywa Maji ya Kutosha, Chini ya Lita 1.5 kwa siku.
3. Kula Chumvi kupita kiasi
4. Kupuuzia Magonjwa madogo modogo hivyo kuyafuga mwilini kwa muda mrefu
5. Kula kiasi kingi cha nyama.
6. Kutokula vizuri na kutosha.
7. Matumizi Mabaya ya Dawa za Kupunguza Maumivu na Dawa nyinginezo
8. Kutomeza dawa/kutotimiza Dozi Inavyopaswa.
9. Unywaji wa Pombe kupindukia.
10. Kutopumzika vya kuzosha.

Kwa Vile mimi si daktari naomba niwasilishe, Tuchukue tahadhari.

Posted by Unknown on 1:18 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

0 comments for "Tabia Hizi za Mazoea Humsababishia Mtu Matatizo ya Figo, Chukua Tahadhari."

Leave a reply

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...